.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

FID Q ADAI ANASTAHILI BANGO YA PICHA YAKE KWA HESHIMA ALIOIPA JIJI HILO


Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amedai kuwa amejaribu kufanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Mwanza ili wajaribu kuweka sanamu za wasanii walionyesha mchango katika mkoa huo. Fid q
Akizungumza na kipindi cha Mkasi TV, Fid Q amesema kwa mchango wanaonyesha wasanii katika nyanja mbalimbali wanahitaji heshima hiyo.
“Juzi nilikuwa Mwanza nikajaribu kukutana na meya, idea ya kumwambia ni kwamba ili sanaa iweze kukua kwa mfano mimi binafsi nimekuwa nikiwakilisha mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa 15, nastahili status Mwanza, unakuja pale Mwanza pale garden unakutana na bango kubwa la Fid Q, sometime inabidi uwape watu idea kwa sababu sisi tupo nyuma ya muda,” alisema. “Kwahiyo ili tufike inatakiwa tukimbie muda ambao wao wanatembea, vitu vidogo tu sanaa unakuza hivyo, kuinspire vizazi vinavyokuja, kwamba ‘okay inabidi nijitume kwa bidii ninaweza nikafika level za kama Fid Q’, labda unapewa mpaka status unapewa mpaka majumba ya kumbukumbu,” aliongeza.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad