Vijana 20 kutoka shindano la kusaka vipaji la Kinondoni Talent Search 2015, wamefanikiwa kutoa wimbo mpya walioupa jina 'kipaji chako Ajira yako' ukibeba kauli mbiu inyobeba maana ya kuanzishwa kwa shindano hilo.
Vijana hao ni kati ya vijana 17510 waliojitokeza katika usahili wa shindano lililofanyika Coco Beach jijini Dar es salaam, mapema mwaka huu.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi Mkuu wa Wilaya ya kinondoni, Paul Makonda alisema vijana hao ndiyo waliopita katika mchujo huo, ambapo mshindi anatarajiwa kupatikana mwezi ujao.
"Shindano hili lina lengo la kuhakikisha kila mkazi wa Kinondoni ananufaika na kipaji chake alichopewa na Mungu. Hata hivyo, ujumbe ulioko katika wimbo huu unawahusu vijana wote Tanzania walio na ndoto zao mtaani kupitia vipaji vyao, lakini wamekata tamaa na hawajui waanzie wapi. Vijana wenzao wameona wawape moyo kwa wimbo huu maalumu." alisema Makonda
Wimbo huo umetayarishwa, umepangiliwa, kutungwa na Peter Msechu, huku ukirekodiwa katika Studio ya Real Studio na Prodyuza Masanja
0 comments :
Post a Comment