UPO msemo uliotawala vichwa vya watu tangu dahari kwamba
wanawake ni tabaka la kukaa nyumbani na kufanya kazi za ndani. Wao jukumu lao
ni kumfurahisha mume na lingine ni kuwaandaa watoto kwa ajili ya kwenda shule
na kufuatilia nyenendo zao darasani.
Happiness Magesse.
Ilivyozoeleka ni kwamba wanawake ni goigoi. Utaona bungeni
kuna wabunge wa viti maalum ambavyo wengi hutafsiri kuwa ni vya upendeleo. Kwa
maana kwamba uwezo wao kushindana kwenye majimbo na kushinda ni mdogo ndiyo
maana wanapewa hivyo maalum kwao.
Katika mitihani, kuna unafuu wa alama za ufaulu kwa
wanafunzi wa kike. Yaani wanaonekana hawana uwezo wa kushindana na wavulana.
Vijijini, wanawake wamekuwa wakitumika kama nyenzo ya kilimo, yaani mama
akalime ndiyo alishe familia, baba akacheze bao au kunywa pombe.
Miaka inakwenda, wapo wanawake wengi ambao wameweza kudhihirisha
kwamba inawezekana kwa jinsi ya kike kuanzisha kazi na kufanikiwa. Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ni mfano wenye
nguvu kwa wanawake kufanikiwa.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mchungaji Getrude Rwakatare na
wengineo, ni kichocheo kinachotoa uthibitisho kuwa wanawake wanaweza. Ni suala
la kuwaamini na kuwapa nafasi, kwa hakika wanaweza kufanya mambo makubwa mno.
Ukiachana na hao, ipo orodha ya wanawake vijana 10 ambao
wanastahili pongezi. Wamepambana katika maeneo yao kiasi cha kupata mafanikio
ambayo yameonesha njia. Inabidi tuwatambue na kuthamini jitihada zao kwa maana
wameendelea kuthibitisha ndivyo sivyo kwa wale waliokuwa wanaamini kuwa
wanawake si lolote kwenye utafutaji.
FLAVIANA MATATA
Mwaka 2007 alipokwenda kushiriki mashindano ya dunia ya Miss
Universe na kushika nafasi ya sita, wengi walidhani huo ndiyo mwisho wake.
Ilionekana hivyo kwa sababu warembo wengi wameshiriki mashindano ya dunia na
baada ya kurudi nchini, hawakusikika tena.
Kwa Flaviana, huo ulikuwa ni mwanzo wa kupiga hatua zaidi
kusaka mafanikio yake. Hivi sasa, mrembo huyo ni mwanamitindo wa kimataifa,
anayefanya kazi na makampuni makubwa ulimwenguni.
EMELDA MWAMANGA
Ni mwanzilishi aliye pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Relim Entertainment inayomiliki jarida maarufu la Kiingereza, Bang. Jinsi
alivyoweza kulisimamisha jarida hilo na kulifanya kuwa maarufu zaidi nchini,
inatosha kumpongeza kwamba ameonesha.
Jina lake asilia ni Judith Wambura. Ni mwanamuziki wa kike
mwenye mafanikio zaidi ambayo chanzo chake ni muziki. Anamiliki bendi na
mgahawa wa kisasa ambao ulimgharimu zaidi ya shilingi milioni 100 kuuanzisha.
Bila shaka Jaydee ameonesha njia kwa wanamuziki wengine wa kike hapa nchini.
MADAM RITA
Kuanzisha kitu wakati mwingine inaweza kuwa jambo rahisi
lakini uimara wa mtu ni pale anapoweza kulisimamia na kufanikiwa. Rita Paulsen
anastahili pongezi kwa namna alivyoweza kuanzisha Shindano la Bongo Star Search
na kulifikisha hapa lilipo. Huyu ni mwanamke kijana aliyeonesha njia ya kweli
ya mafanikio.
RAHMA AL-KHAROOS
Anamiliki Kampuni ya RBP Oil & Industrial Technology.
Uwezo wake uliweza kuwashtua wengi pale alipoweza kujitolea mamilioni ya fedha
kuiwezesha Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars. Mwanamke huyu ni mfano tosha
kwamba inawezekana kama tu utaamua kupambana.
SHEAR NASSA
Anamiliki maduka ya Shear Illusions, vilevile ana jarida
linaloitwa Shear Hair & Beauty. Ukubwa wa maduka yake, heshima na umaarufu
wake kwa uuzaji wa vitu vya urembo ni kielelezo cha kumthibitisha Shear kwamba
ni mwanamke kijana aliyefanikiwa, kwa hiyo ameonesha njia.
KHADIJA MWANAMBOKA
Mbunifu wa mavazi wa kike mwenye umaarufu kuliko wanawake
wote nchini. Ameanza harakati zake akiwa na umri mdogo na kwa alipofikia hivi
sasa, ameshaonesha njia kwa wanawake wengine nchini. Jambo muhimu ni kusimamia
fani yako mpaka kuifikisha kwenye kiwango bora. Khadija alipofikia kwa ubunifu
wa mavazi, anastahili pongezi
FINA MANGO
Alipata umaarufu mkubwa kwenye fani ya utangazaji wa redio
lakini alipoamua kuanzisha kampuni yake ya One Plus, ameweza kupata mafanikio
makubwa. Tenda ya kuratibu na kusimamia Tuzo za Muziki Tanzania (Tuzo za Kili)
kwa miaka mitatu mfululizo imedhihirisha ubora wa kampuni yake
Huyu ni mama
Asha Baraka mkurugenzi
ASSET hakika ni
mpiganaji sana wa
maendeleo ameweza kuwaajiri
vijana wengi sana
kupitia kampuni yake
ya Asset ambayo
inamiliki bendi ya
twanga pepeta. licha hivyo
ASHA BARAKA maaarufu
kama iron lady
ameweza kusaidia vijana
wengi kupata mafanikio
ya mziki kupitia
bendi yake twanga
pepeta
0 comments :
Post a Comment