.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Sitti Mtemvu ni "Miss Tanzania 2014". Full Stop


Mshindi wa Miss Tanzania Sitti Mtemvu"katikati" pamoja na warembo wengine, kulia kwake ni mshindi wa tatu Jihhan Dimachk na kushoto kwake ni Lilian Kamazima mshindi wa pili.

Ushindi wa Bi Sitti Abbas Mtemvu katika kinyang'anyiro cha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania ya mwaka 2014 umezua shutuma juu ya uhalali wa mrembo huyo kuvikwa taji hilo.
Siku chache baada ya kutangazwa kwake kuliibuka shutuma mbalimbali dhidi ya Bi Sitti na kumwondolea vigezo vya umalkia huo wa urembo.Tuhuma hizo zilianza kuzagaa katika mitandao ya habari ya kijamii zikiwemo shutuma za kufanyika udanganyifu wa umri.

mkurugenzi mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga
Kamati ya kuandaa mashindano hayo, siku ya Jumanne imelitolea ufafanuzi suala hilo,mjini Dar es Salaam, ambapo mkurugenzi mtendaji wa kamati hiyo, Hashim Lundenga amesema, Sitti ndiye mshindi halali wa mashindano hayo ya mwaka 2014, na kwamba shutuma dhidi yake hazina msingi wowote zaidi ya kuwa uzushi: "Mimi nasema shutuma zote zilizotolewa hapa ni shutuma za uongo, kwa sababu kulingana na taratibu nilizozieleza hapo awali, sisi kama kamati kama waandaaji wa Miss Tanzania hatuna matatizo yoyote" anasema Bwana Lundenga.

Sitti Mtemvu "Miss Tanzania 2014"
Akizungumzia tuhuma kwamba Bi Sitti alidanganya umri kuwa ana miaka 18, mkurugenzi mtendaji wa kamati ya Miss Tanzania, Bwana Lundenga ameshangazwa na uzushi huo, akisema mrembo huyo hajawahi kutaja umri huo kama ndio umri wake. "hakuna mahala popote alipozungumza kuwa ana miaka 18...Kwa hiyo ni rumours ambazo zinaendelea tu na wameshindwa kuhakikisha"
Kwa ufafanuzi wa waandaaji wa mashindano hayo, Sitti Abbas Mtemvu ni mshindi halali wa Miss Tanzania 2014 na ndiye anayetarajiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya mrembo wa dunia ya Miss World yatakayofanyika 2015.

Credits:BBC SWAHILI
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad