Klabu ya Manchester Uniter ya Uingereza imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Gareth Bale (25) baada ya Manchester United kushindwa kumrudisha Ronaldo (29) Manchester. (imeripoti Daily Star)
Kocha wa Queens Park Ranger, Harry Redknapp amemwambia kiungo wa timu hio Adel Taarabt (25) kwamba hatouzwa katika dirisha dogo la Januari labda mpaka pale itakapotokea timu ambayo itafikia bei wanaoitaka. (Imeripoti Daily Mirror)
Klabu ya Uingereza, Sunderland imetupilia mbali ombi la klabu ya Scunthotpe la kumsajili mshambuliaji Duncan Watmore (20) kwa mkopo (Imeripoti Sunderland Echo)
Klabu ya Arsenal wataingia gharama ya kurekebisha viti zaidi ya 100 katika kiwanja chake baada ya mashabiki wa Galatasaray kuviaribu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliochezwa Jumatano iliopita, Arsenal walishinda 4-1 (Imeripotiwa na Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge (25) ambae ametia sign ya mkataba wa miaka 5 wa kuitumikia Liverpool amesema kwamba angependa kuwa muigizaji baada ya kustaafu kucheza mpira (Imeripoti Esquire)
0 comments :
Post a Comment