STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ameanika ukweli kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mchumba wake Malick Bandawe baada ya kuwagundua wanawake wawili aliozaa nao mbali na yeye.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Rose aliamua kufungasha virago vyake na kurudi kwa mama yake mzazi maeneo ya Kigogo baada ya kugundua kwamba mchumba’ake huyo alizaa na wanawake wawili tofauti na yeye ambaye ni wa tatu.
“Alichokizungumza Malick kwamba alishamuweka chini Rose na kuzungumza naye si kweli, ila yeye Rose aliamua kurudi kwao baada ya kugundua jamaa ana wanawake wawili aliozaa nao kabla yake,” kilisema chanzo hicho.
Akaongeza: “Kile kilichosemwa na Malick kuwa anasikitika kuona mtoto wake anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine ni kujitetea tu lakini ukweli ni kwamba mwanaye analelewa na yeye mwenyewe kwa sababu yuko nyumbani kwa mama yeke.”
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Rose kwa njia ya simu yake ya mkononi, alipopatikana na kusomewa madai hayo alikata simu huku akisikika akisema hayuko tayari kufunguka lolote kwa sasa
0 comments :
Post a Comment