ITV imefika katika eneo hilo na kukuta watu hao wengiwao ni watoto
wakiwa bado wanaendelea kuteseka na hali ngumu wanayoipata kulala nje
na kunyeshewa mvua ambapo wakiongea kwa uchungu huku wakionyesha hati
halali ya umiliki wa nyumba yao wameiomba serikali kuwasaidia.
Baba mzazi wa familia ambaye anadaiwa kuuza nyumba hiyo Fredinandi
Kainyingi amesema watoto wake ndiyo wamiliki halali wa nyumba hiyo
licha ya kutoa ushahidi wa kutosha juu ya umiliki wa nyumba lakini
vyombo vinavyohusika bado vinawanyima haki na kushindwa kujua nini hasa
lengo la vyombo hivyo.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Jumahamsini Omari Makiluka na majirani
wamesema wanajitahidi kuwapa misaada ya chakula ingawa hawanauwezo wa
kuwapa huduma ya ladhi watu wote hao na wameimba serikali na mashirika
ya haki za binadamu kuingilia kati kuona uwezekano wa kuwasaidia.
Source: ITV
0 comments :
Post a Comment