Mlinda mlango wa kikosi cha kwanza cha washika mtutu wa jiji la London ‘Arsenal’, Wojciech Szczęsny amepigwa faini ya paundi 20,000 za Uingereza kwa kitendo chake cha kukutwa akivuta sigara muda mfupi baada ya kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Southampton.
Kufuatia kitendo cha mlinda mlango huyo, meneja wa klabu iyo Arsenal Wenger ameamua kumpa adhabu hiyo kuwa fundisho la kufanya atambue uwajibu wake kwenye klabu.
Msala kama huo wa uvutaji sigara uliwahi kumkumbuka kiungo wa kimataifa wa klabu iyo, Jack Wilshare pamoja na nahodha wa zamani ‘William Gallas’ ambapo picha zao zilitolewa kwenye vyombo vingi vya habari.



No comments:
Post a Comment