.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Msanii Tyga akana uhusiano wake na Kylie, Afunguka mengi kuhusu Cash Money

Tyga

Tyga anashow mjini Brooklyn katika tour iliopewa jina la "Between the Sheet Tour," hivyo akaona apitie katika radio ya Power 105.1 na kuhojiwa katika kipindi cha "The BreakFast Club" siku ya Jumanne, baada yakuona mambo mengi yasiokweli yakisemwa kwenye twitter akaunti yake.

Tyga aliweza kueleza yote kuhusu uhusiano wake kimapenzi na Kylie Jenner pamoja na beef yake na Drake. 
"Jana nimekaa naona mambo mengi yanasemwa kwenye twitter, nikaona nije ili nionge japo mie sio mtu wakuongea maisha yangu binafsi sana." Alisema Tyga



Ikumbukwe wiki iliopita, Amber Rose alihojiwa katika kipindi hicho na kumtolea maneno Tyga kisa ana uhusiano na mtoto wa miaka 17 ambae ni Kylie Jenner (Kylie ni miongoni mwa Kardashians). ila kwa mujibu wa Tyga ni kwamba wawili hao hawana uhusiano wa Kimapenzi.

"Sina uhusiano na Kylie, kwaio nataka kuimaliza hio mada," alisema Tyga. "Nataka nieleweke kwa kila mtu kwamba sikuacha familia yangu ili niwe na Kylie."
Anatunza heshima ya uhusiano wake na Blac Chyna. Wachumba hao walibahatika kupata mtoto aitwae King Cairo mwenye miaka miwili. "Mambo yalikua hayaendi sawa katika uhusiano wetu tukaamua kuachana ili tukuze mtoto mwenye hisia imara," alisema Tyga 



Tyga alizungumzia kuhusu Cash Money Pia. 

"Biashara haikuwa tu sawa. sio kosa la Wayne, Unaona hali inayotokea sasa hivi." alisema Tyga
"Kama kila kitu kipo poa na kila mtu ana mamilioni, inabidi nihakikishe kwanini biashara haiendi sawa."
"Unajua Label inawasanii wakubwa wana Drake, Nicki, Wayne na mimi wenyewe kwaio wasanii wengi, labda inakuwa ngumu kuwaHandle." 
Tyga alitakiwa kutoka kwenye deal na label ya Cash Money mwezi December ili aachie album ya "The Gold" kivyake mwezi January, ila hilo swala halijafanyika mpaka sasa. 
Kwa sasa yeye na Drake wanaendelea na mabishano, Baada ya drake kumDis kwenye "6PM in New York," kisha Tyga akimwita drake "B*t*h."
"Binafsi sina mazoea nae kwasababu ya uzoefu niliopata nae binafsi," Tyga alisema katika kipindi na radio. "mziki wake ni mzuri, haikataliki. ndo mda wake."
Chuki yake kwa rapa huyo wa kutoka canada inatokana na uzoefu binafsi.
"Sio beef kivile, ni uzoefu niliopata nae kwenye, simu, na mambo kama hayo." alisema Tyga
Ikija kwenye kurap, alikubali Drake ni mwenye akili kuzidi yeye, ila aliongezea kwa kusema, "Nina nguzo pia mimi."
Ukiachana na vinavyosemwa, yeye hana tatizo na Nicki Minaj, ila anakubali walijibizana kisa nyimbo ya Nicki "Truffle Butter."
"Mimi na Nicki tuligombana kisa kitu cha kijinga tu," alisema Tyga . "Hivyo ndivyo kaka na dada wanafanya. wanagombana. Sina kitu chochote juu ya Nicki."
Mtu ambae yupo nae safi sana ni Chris Brown. Wakati wa kesi yake, "Alifikia kiasi cha kwamba hakutaka kufanya mziki tena kisa watu wanamshabulia sana," alisema Tyga. "Siku muhukumu yeye. Nilimwangalia, 'wewe Chris Brown. Wewe Mike Jack. Unatakiwa kufanya muziki."
Tyga alienda mpaka mjini Virginia na kukaa nyumbani kwa Chris kwa miezi miwili na kurecord "Fan of a Fan mixtape. "nilikua nae katika kipindi wamemuacha."

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad