.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Pambano La Dunia: MayWeather vs Pacquiao kupanda Ulingoni tarehe hii


Hatimaye tarehe ya pambano la wakali wawili wa boxing duniani Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lilokuwa likisubiriwa kwa hamu imejatajwa na sasa wawili hao watashuka uliongoni  tarehe  2/May/ 2015 huko Las Vegas Marekani.


Hii imethibitishwa usiku wa jana mara baada ya mmarekani Mayweather kuposti katika mitandao ya kijamii picha ya mkataba wa makubaliano kati yake na Pacquiao ukiwa umesainiwa na wawili hao.



Pambano hilo lililosubiriwa na mashabiki wa mchezo huo kwa miaka mingi linathamani ya dola za kimarekani milioni 250.
 "Kuwapa mashabiki kitu walichotaka kukiona ndiyo lengo langu. Hilo litakuwa tukio kubwa la kihistoria katika michezo. Mashabiki wa boxing na michezo watashuhudia maajabu May 2, siku zote nimekuwa bora na hii ni nafasi nyingine kubwa ya kuonesha ubora wangu na kufanya kile ninichoweza kufanya ambacho ni ushindi." amesema Mayweather.


Kwa upande mwingine Mfilipino Manny Pacquiao amesema kuwa amefurahi kupata nafasi ya kuwapa mashabiki kitu walichokuwa wanakisubiri kwa muda mrefu na wanastahili. 

"Pambano hili ni kwa ajili ya mashabiki wote duniani waliokuwa wanasubiri kwa muda mrefu na pia kuleta furaha kwa wafilipino wenzangu. " amesema Pacquiao.

Mayweather ameshinda mapambano yote 47 aliyowahi kucheza huku Pacquiao akipoteza mara 5 katika mapambano 64 aliyocheza mpaka sasa.
Pambano hili limekuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki mbalimbali duniani kutokana na wawili hao hawajawahi kukutana ulingoni hata mara moja.


Source: WorldSports14

Tuachie Comment Yako 
kisha
Usisahau kutufollow ili habari  kama hizi zisikupite Pindi tu tatakapo ziweka.

Like our  Facebook page CLICK HERE
Follow Twitter CLICK HERE
Follow Instagram CLICK HERE
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad