Mchezaji wa klabu ya Swansea City inayoshiriki Ligi kuu Uingereza, Bafetimbi Gomis amezimia uwanjani katika mechi ya Tottenham leo Jumatano na kuhitaji huduma yakwanza.
Mfaransa huyo alianguka chini katika uwanja wa White Hart Lane bila ya mtu yeyote kuwa karibu yake, alitolewa nje kwa machela.
Gomis (29) alitolewa uwanjani akiwa hajitambui.
Usajili huo wakati wa dirisha kubwa kutoka Lyon alizimia wakati wachezaji wakijipanga kuanza mpira baada ya Nacer Chadli kuipa Totenham ushindi wa goli lakwanza.
Gomis alihudumiwa uwanjani kwa dakika 4 kisha kutolewa nje na machela, yakwamba hajitambui na alikuwa akipumua kutumia Oxygen Mask.
Gomis ana historia yakuanguka, kocha wake wazamani akiwa Lyon Jean-Michel Aulas amesema walipata hofu ya mshambuliaji huyo mnamo mwaka 2009
0 comments :
Post a Comment