Mchezo huo uliisha kwa sare ya bila kufungana, huku Kipa wa Athletico Madrid "J. Oblak" akionesha kiwango kizuri baada ya kuokoa mashambulizi mengi ya hatari.
Real Madrid walimiliki mpira sana na kupeleka mashambulizi mengi sana, labda tatizo lilikuwa kwa washambuliaji kwani Mshambuliaji wao, Benzema alikuwa out of form kwani alionekana akikosa nafasi nyingi za wazi pia kupiga vichwa pembeni mpaka pale mwalimu Ancelotti alipo amua kumtoa na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mshambuliaji Isco.
Kwa Upande wa Mechi ya Juventus dhidi ya Monaco, Mechi iliisha kwa wenyeji Juventus kushinda Goli Moja na kuipa wakati mgumu Monaco ambao wanatakiwa washindi goli 2 katika kiwanja chake cha nyumbani katika mechi ya marudiano dhidi ya Juventus ili waweze kuvuka hatua hii, Mpaka sasa Juventus wapo katika nafasi nzuri ya kuingia Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya endapo wasipo ruhusu goli katika mechi ya Marudiano ikiwezeka ni kuongeza magoli kama si Goli tu.
Unazungumziaje Mechi hizi Mbili, tukiwa tunasubiri Mechi zao za Marudiano.. Tuachie Comment Yako ....
0 comments :
Post a Comment