Guardiola anarudi Camp Nou kwa mara yakwanza tangu kuwanongoza Los Cules kuchukua Ubingwa wa Ulaya mara 2 ila leo anacheza kushinda na mabingwa wa Ujerumani.
Kocha mkuu wa Bayern Munich, Pep Guardiola ametangaza 'haiwezekani' kusimamisha Lionel Messi.
Mhispania huyo anawaongoza mabingwa wake wa Ujerumani dhidi ya pambano na Messi na Barcelona leo Jumatano usiku.
Mara yake yakwanza kurudi akiwa kocha mpinzani tangu miaka 4 alipo waongoza kubeba makombe 14.
Kocha huyo mwenye miaka 44 anajua kwamba kama Bayern itapita kuingia fainali ya 2 ndani ya miaka 3 basi watahitaji kumdhibiti Messi, ambae yupo na Luis Suarez na Neymar ameshiriki zaidi ya magoli 100 msimu huu kwa Barcelona.
Pia Guardiola anaamini kwamba upande wake hauwezi kudhibiti uwezo wa mchezaji huyo bora wa dunia mara 4 na vyovyote atakavyojaribu kudhibiti uwezo wa Messi, basi lazima kipaji kijieleze.
"Kama Messi atakuwa kama navyodhani, hakuna beki atakae weza kumsimamisha, haiwezekani," alieleza Guardiola
"Wakati Messi yupo kwenye Form, kama sasa, hakuna sytem ya ukabaji wala kocha anaeweza kumsimamisha.
"Kumuwekea kikwazo ni tofauti - Kuwa muangalifu na toa mpira kwake.
"[Japokuwa] wanafaida. nawajua, ila siwezi dhibiti vipaji vyao. Unaweza fikiria nini Messi au Neymar watafanya, ila kipaji kina danganya."
Kwa sasa Bayern wamekubwa na janga la Majeruhi, huku baadhi ya kikosi cha kwanza pia - Arjen Robben na Franck Ribery - Nje
Ila, Robert Lewandowski anatarajiwa kuanza , Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuva mask, na Guardiola ametangaza kumpa kila nafasi yakucheza.
"Lewandoski amefanya mazoezi. Nitaongea nae. Tunahitaji wachezaji wote wawe asilimia 100. Nahitaji kujua anajisikiaje na Mask.
Tuambie nani atafika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
1- Barcelona
2- Bayern Munich
Tabiri Matokeo au wafungaji unaweza jishindia zawadi kutoka kwa wadhamini wetu........ Tuachie Comment
0 comments :
Post a Comment