.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

De Gea aanza kuanga Man United





MADRID, Hispania
MLINDA mlango David De Gea amewaambia wachezaji wenzie wa Manchester United kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Real Madrid katika msimu ujao.

Hatima ya baadaye ya mlinda mlango huyo katika Old Trafford iko kwenye hatihati kutokana na Madrid kuonesha nia ya kutaka kumsaini ili achukue nafasi ya Iker Casillas.

Wengi kati ya wachezaji wenzie, De Gea katika timu ya wanaamini kuwa nyota huyo anaweza kuondoka na kumekuwa na mjadala.

Gazeti la Sportsmail lilisema mapema wiki iliyopita kuwa Real inataka kutuma ofa yake ya kwanza ya kiasi cha pauni milioni 13 kwa mchezaji huyo mwenye umei wa miaka 24.



Man United inaweza kugoma kupokea kiasi hicho ili nyota wao aondoke Old Trafford.

Kwa upande mwingine, Real inaamini kuwa itampata De Gea ikijua kuwa moyo wa mlinda malango huyo umejiandaa kurejea katika mji mkuu wa Hispania.

Kama De Gea ambaye alikuwa msimu mzuri United na kuisaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya nne tofauti na msimu uliotangulia ilipoishia nafasi ya saba, akiondoka itafanya kocha Louis van Gaal atafute mlinda mlango mwingine wa kuziba nafazi yake.

Mlinda mlango  wa Tottenham, Hugo Lloris anatajwa kuwa anaweza kuziba nafasi yake ya de Gea katika kikosi cha United, timu yake inadaiwa inaweza kutaka dau la pauni milioni35 ili kumwachia mlindamlango huyo anayeidakia pia timu ya taifa ya Ufaransa.

Mlinda mlango wa Atletico Madrid, Jan Oblak  naye anatajwa kuwemo kwenye rada ya United United.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad