.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Chelsea, Mancity zamwinda Song




LONDON, Uingereza
KLABU ZA Chelsea na Manchester City zimefanya mazungumzo ya kumsajili kiungo Alex Song kutoka Barcelona, imesema mtandao wa Sky Sports.

Klabu hizo zinamtaka Song kwa kuwa anafuzu kuwa mchezaji wa nyumbani licha ya kuichezea Cameroon.

Song ambaye ameichezea West Ham msimu uliopita kwa mkopo ana miaka miwili ya kandarasi yake na Barcelona.


Hata hivyo West Ham ina matumaini ya kumsajili mchezaji huyo, Sky inaamini kwamba kuna klabu kadhaa  zina hamu ya kumnunua ikiwemo City na Chelsea.

Nyota huyo mwenye 27 ambaye aliichezea klabu ya Arsenal kwa miaka sita kabla ya kuelekea Barcelona miaka mitatu iliopita alicheza mechi 28 katika West Ham msimu uliopita.

Barcelona iliomnunua mchezaji huyo kwa pauni milioni 15 inaaminika kutaka kumuuza huyo kwa pauni milioni 5.


Mkataba wake katika klabu hiyo ya Nou Camp inaaminika kuwa analipwa kitita cha pauni 70,000 kwa wiki.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad