.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Kocha wa Taifa Stars akalia kuti kavu, Asipoitoa Uganda kufungasha Virago




Raisi wa Shirikisho la Mpirawa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amesema msimamo wao ni ule ule kuwa kocha Mart Nooij akishindwa kuiwezesha timu ya Taifa (Taifa Stars) kuiondoa Uganda katika mechi ya kuwania kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN), watasitisha mkataba naye.



Akizungumza Dar es salaam jana, Malinzi alisema tayari Kamati ya Utendaji ya TFF imeshampa muda kocha huyo endapo atashindwa kufanya vizuri katika mchezo wao wa Jumamosi utakaofanyika Zanzibar dhidi ya Uganda na mechi inayofuata itakayofanyika Julai 4, mwaka huu ataondokea huko huko.

Alisema wao wanachotaka waitoe Uganda, endapo atashindwa hawataweza kuendelea naye.
"Nadhani kamati yetu ya utendaji ilikaa na kuamua hilo, endapo atafungwa Zanzibar na mechi ya marudiano nchini Uganda, basi atatuachia timu yetu na kuondoka huko huko," alisema Malinzi.

Mart Nooij (Gallo Images)
Alisema kama TFF, imesikitishwa na matokeo ya mwishoni mwa wiki ambapo kikosi cha Stars kilifungwa mabao 3-0 dhidi ya Misri.

Malinzi alisema wanajua kila Mtanzania aliitaji matokeo mazuri, lakini wenzao waliwazidi kwa kupata ushindi wa mabao hayo matatu. Alisema hata hivyo kwa upande wao wamejipanga vizuri kuhakikisha kikosi chao kitakuwa katika mazingira yote ya ushindi, labda itokee kwa upande wa benchi la ufundi chini ya kocha wao huyo.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad