.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Madaha ajiongeza katika filamu



Charity James
MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya na filamu za kibongo nchini, Baby Madaha, amesema baada ya kimya kirefu sasa ameamua kujikita katika filamu na kuwa mtayarishaji wa filamu hizo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Madaha alisema kuwa ameona si vema kufanya muziki na filamu pekee, ni bora ajishughulishe na mambo mengine kama utayarishaji wa filamu na ndio maana akaja na wazo la kufungua kampuni yake.



Alisema muziki una changamoto nyingi na kudai kuwa wasanii wengi wanazaliwa na vipaji kila siku, hivyo akaamua kufungua kampuni ambayo itakuwa inatengeneza filamu na kazi nyingine.

Alisema ndoto yake katika tasnia ni kuwa mwandaaji mkubwa wa filamu na anaamini ataitimiza baada ya kufanikiwa kufungua kampuni yake mwenyewe ambayo atakuwa akiisimamia.



"Baada ya kufungua kampuni yangu ya kuandaa filamu naamini nitatimiza ndoto yangu ya kuwa mwandaaji filamu bora katika bara la Afrika," alisema.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad