Nyota wa filamu nchini, Kajala Masanja, amesema hajamuomba radhi rafiki yake wa zamani, Wema Sepetu, lichaya kutuma ujumbe wa hisia wa kusifu utu wa mshindi huyo wa taji la Miss Tanzania 2006.
Akizungumza katika kipindi cha television cha 'Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV kila ijumaa kuanzia saa 4:00 usiku, kajala aliendelea kutokuwa tayari kutaja chanzo cha ugomvi wake na rafiki yake huyo wa zamani
"Kuna mambo hauna sababu ya kuyataja hadharani alisema Kajala na kusisitiza kwamba ujumbe aliouandika wa kumshukuru Wema kwa wema wake haumaanishi kwamba amemuomba radhi. "Siku nikiamka, nikaona kweli nimekosea Wema nitaenda getini kwake kugonga na kuomba radhi, lakini si kwa kupatanishwa na watu," alisema Kajala.
katika ujumbe wake kwenye Instagram mwezi uliopita, Kajala aliandika:
"
BINADAMU TULIUMBWA KUISHI KATIKA MISINGI YA UBINADAMU NA SIO UNYAMA KAMA WAISHIVYO WANYAMA WA PORINI LEO NAOMBA KUSEMA KUTOKA MOYONI MWANGU.. NAJUA KABISA NINA WAZAZI WANGU NDUGU ZANGU NA ZAIDI SANA MUNGU WANGU ILA KUNA WATU MPAKA NAKUFA KAMWE SINTOWASAHAU KATIKA KUTA ZA MOYO WANGU KATIKA KIPINDI CHANGU KIGUMU NILICHOPITIA MLIKUWA NEMBO NAMBONI KUBWA KATIKA KUOKOA MAISHA YANGU... NAPENDA KUSEMA KUWA HATA KWA HAYA YOTE TUNAYOPITIA BADO NI MADOGO SANA KUFICHA THAMANI YENU MLIYOIJENGA JUU YANGU..NAKUMBUKA SANA MLIPOJITOA KWA AJILI YANGU MLIPOJINYIMA KWA AJILI YANGU MLIPOPIGANA KWA AJILI YANGU,MLIVYOFEDHEHEKA KWA AJILI YANGU YOTE HAYO NAYAKUMBUKA NA NAMSHUKURUU MUNGU KWANI NAONA KABISA MLILETWA DUNIANI KWA SABABU NYINGI NA MOJA YA SABABU ILIKUWA KUNIOKOA KATIKA KIPINDI KIGUMU KATIKA MAISHA YANGU.LEO HII TAREHE 25.5.2015 NAPENDA KUSEMA KWA UMMA NA ZAIDI KWA MUNGU WANGU KUWA NAWATHAMINI NAWAPENDA NA NASHUKURUUU SANA KWA YOTE MLIYOFANYA JUU YANGU.. NAWAOMBEA KWA MUNGU MUENDELEE NA MOYO HUO HUO KWANI NAAMINI KUNA WENGI BADO WANAWATEGEMEA ILI KUKOMBOA MAISHA YAO KWA WAKATI ALIYOPANGA MUNGU
HATA KITABU CHA DINI KILISEMA KUWA "huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona" NAJUA SIKU MOJA TUTAISHI KAMA ZAMANI.. AHSANTENI
Source: Nipashe
0 comments :
Post a Comment