Mbunge Sugu akiwa na mwanae Sasha
Kwenye kilichosikika jana June 25 2015 toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma ilikuwepo pia ishu ya Mbunge Martha Mlata kuanzisha mjadala kuhusu amri ya Mahakama kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi Sugu akabidhiwe mtoto wake ambae amezaa na Faiza Ally kutokana na Mbunge huyo kuonekana kutoridhwishwa na malezi ya mtoto akiwa kwenye mikono ya mama yake.
Mheshimiwa Mbunge Mlata Alisema Haya:
"Tuna Mbunge mwenzetu
amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani
kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu
mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake"
Ombi likapokelewa kwenye
meza ya Naibu Spika leo June 26 2015 >>>”Nimepokea ombi maalum
la kuwasilisha maombi binafsi kutoka kwa Mbunge Joseph Mbilinyi kwa hiyo
namruhusu” >>> Naibu Spika Job Ndugai.
“Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo”
“Hakutaja jina la Mbunge
aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata
hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa mtoto kuwa ni
Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond
Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa
kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye
ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia“
“Watu wazima hawapendelei
kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata
Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo
yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika“
“Mimi ni mmoja wa watu
wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu
uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha
ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote
nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule
Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza
ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito“
“Mwanamke anayedaiwa kuwa
mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake
zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu
wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers
zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo
haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge“
“Nilienda Mahakama ya
Mwanzo Manzese, niiwashilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza
kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama
iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili
nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya
Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama
anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
“Mashauri haya hayakupaswa
kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na
Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa haki,
mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa
nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu
usiendelee zaidi ya hapa” >>> Mbunge Joseph Mbilinyi.
0 comments :
Post a Comment