.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Mwana FA: Wasanii wa nje hawana msaada

                    
Rapa wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA', amesema haoni faida yoyote kufanya kazi na msanii kutoka nchi nyingine lakini uwezo wa kupata wasanii wa kufanya nao kazi upo.

Akizungumza Dar es salaam jana, Mwana FA, alisema anafanya muziki kwaajili ya watanzania hivyo hawezi kufanya kazi na msanii kutoka taifa lingine na watanzania wakashindwa kuelewa anachoimba.



Alisema ikitokea msanii wa nje akitaka kufanya kazi na yeye atafanya naye lakini sio yeye ahangaike kumtafuta kwaajili ya kufanya naye kazi.

"Kama itatokea nimeenda kufanya kazi na msanii kutoka nje basi nitakuwa nataka kutoka kama msanii aliyehitajika kutoka bongo sio kwasababu mimi nataka kufanya tu sioni kama inafaida kwenye muziki wangu," alisema.

Mwana FA alisema lugha anayoitumia kufanya muziki inafanya watu kusikiliza kwa umakini zaidi kuliko akitumia lugha nyingine.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad