Juma Nature
na Charity James
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Nature, amesema tamasha lake la miaka 16 alilolifanya hivi karibuni, limetoa majibu kuhusu ukomavu wake katika tasnia hiyo.
Amesema kwa muda mrefu watu wamekuwa wakimjengea fitina ili ashuke kimuziki lakini sasa jibu wamelipata.
Akizungumza Dar es Salaam, juzi alisema watu wameendekeza majungu na chuki na ndio maana uwezo wake unaonekana kusahaulika na anajua kuna watu wanataka kumshusha lakini majibu wamepata kupitia tamasha lake alilofanya hivi karibuni.
Alisema safari ndio imeanza na wasanii wachanga anadhani wamejifunza nini wanatakiwa kufanya ili waendelee kuishi na watu na sio kubweteka na kusahau majukumu yao katika jamii.
Nature alisema kinachofuata baada ya tamasha lake ni kuzunguka mikoani kuzungumza na mashabiki pia kufanya matamasha ambayo yatawapa fursa wasanii chipukizi kuweza kutoa burudani na kuonesha vipaji vyao.
"Muziki wa sasa umetawala majungu watu wanaacha kufanya muziki wanaanza kumfuatilia mtu anafanya nini, mtu kama unakipaji unacho tu, mimi ninakipaji na najua ninachokifanya katika muziki hivyo wapenzi wa kazi zangu wakae mkao wa kula," alisema.
0 comments :
Post a Comment