Simba yaita vyombo vya dola kuchunguza mkataba wa Ramadhani Singano 'Messi'

Uongozi wa klabu ya Simba umesema upo radhi vyombo vya dola vichunguze
mkataba wao na mchezaji Ramadhani Singano 'Messi', ili kuweza kubaini ukweli na
kutatua utata unaoendelea kwasasa.
Messi atakuwa mchezaji wa pili Simba mkataba wake kuchunguzwa na vyombo vya
dola baada ya ule wa Athuman Idd 'Chuji'
kudaiwa kufojiwa saini kama ilivyo sakata la Messi, kipindi anataka kuihama
klabu hiyo mwaka 2008/2009.
Akizungumza Dar es salaam jana, Ofisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara,
alisema vyombo hivyo pekee ndivyo vinavyoweza kulimaliza suala hilo na wapo
tayari kwa wao kufika na kuchunguza. "kila mmoja amekuwa akizungumza yake, lakini ukweli sisi tunaendelea
kumtambua kama bado ni mchezaji wetu,
tuna mkataba naye wa mwaka mmoja lakini uthibitisho zaidi utaamuliwa na
vyombo hivyo," alisema Alisema licha ya kusubiri uhakika huo, lakini wapo tayari kwa tamko lolote
kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuhusiana na hilo, kwani wao pia wanakopi
ya mkataba huo."Tupo tayari kwa majibu yoyote tutakayopewa baada ya uchunguzi huo
kukamilika, kwani tunataka kuona kila kitu kinafanyika kwa misingi ya
haki," alisema
Alisema kitendo hicho cha Messi kimewasikitisha uongozi wote kwani si
halali kwa yeye kulalamika kitu ambacho si sahihi na hiyo ni kutokana na
kuponzwa na wakala wake, huku wakishangazwa na mchezaji huyo kuwa na wakala
wakati amekuzwa na kupandishwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kuhusiana na suala ya yeye Msemaji kwenda nchini Afrika Kusini kwenye
michuano ya Cosafa kusaka wachezaji ambao watasajiliwa na timu hiyo, alisema
wapo wachezaji ambao amewaona kutoka nchi mbalimbalina ameshafikisha suala hilo
kwa uongozi.
"Ni mapema sana kwa sasa kusema nchi wanazotokea wachezaji hao, ila
nimekamilisha hatua muhimu niliyotumwa na uongozi sasa kazi nimewaachia
wao," alisema
Alisema kwa upande wa usajili wanaendelea na mchakato huo kwa kufuata
maelekezo ya kocha Goran Kopunovic, ambapo pia taratibu za kupatikana kwa kocha
mpya au Goran kuendelea na mkataba zitafahamika ndani ya siku tatu kuanzia
sasa, huku wachezaji watakaotemwa watawekwa hadharani Ijumaa. Source Mtanzania
No comments:
Post a Comment