Wednesday, 3 June 2015

Sony Music yakanusha taarifa za kuzuia nyimbo za Beyonce

Kampuni maarufu ya Sony Music imekanusha uvumi kuwa ina mipango wa kuzuia nyimbo za mwanamuziki Beyonce kuingiziwa kwenye tovuti ya Tidal.


Mkurugenzi mtendaji wa Sony, Doug Morris amekanusha vikali uvumi kuwa kuna mpango wa kuzizuia nyimbo za mwanamuziki huyo kuingizwa kwenye tovuti ya Tidal inayomilikiwa na mumewe, Jay Z.


Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ.com, Morris alisema kuwa hakuna mpango wa kuhitaji fedha kutoka kwa Jay Z anayemiliki tovuti hiyo inayojihusisha na masuala ya muziki kwa madai kuwa wawili hao ni marafiki. Vyombo mbalimbali vya habari jana vilitaarifu kuwa label hiyo imetishia kuzuia nyimbo za Beyonce kuingizwa katika tovuti ya mumewe kwa kuwa bado ana mkataba na kampuni hiyo.
"Siyo kweli, hakuna jambo hilo, tunafanya kazi vizuri na Jay Z kwa miaka mingi sasa hatujazuia na hatuna mpango wa kufanya hivyo wala kudai fedha ," alisema Morris. 

No comments:

Post a Comment