Wanachama wa klabu ya Simba waliopo jijini Dar es salaam wanatarajia kuwaombea dua wenzao waliofariki msimu huu katika hafla itakayofanyika katika Msikiti wa Idrissa , kariakoo siku ya Jumapili
Kiongozi wazamani wa timu hiyo, Said Rubeya, aliyeongozana na mwezake Rajab Mlanzi, walithibitisha kuwapo kwa tukio hilo katika ofisi za NIPASHE Mikocheni juzi (Jumanne) mchana.
Rubeya alisema kuwa dua hiyo ni ya kuwaombea heri wanachama hao ambao wengi ni wale waliofariki katika ajali mkoani Morogoro wakielekea Shinyanga kwenye mechi dhidi ya Stand United.
Rubeya alisema sala maalum na Maulid hiyo ya Jumapili itaongozwa na sheikh Suleima Kilemile na masheikh wengine wakiwamoHussein Ismail, Anwar Jongo na Abdullah Kazuba. Aidha, Mbunge wa Ilala, Idd Hassan 'Zungu' atakuwa mgeni wa heshima katika tukio hilo.
"Timu yetu imekubwa na misukosuko mingi katika msimu uliomalizika hivi karibuni, ikiwamo kufiwa na wanachama wenzutu (Ukawa)," alisema Rubeya.
Alisema ni vyema kuwaombea heri wanachama hao ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mwaliko wa jumla umetolewa kwa wanachama wote wa Simba kuhudhuria maombi hayo maalum yanayotarajiwa kuanza baada ya sala ya adhuhuri na kumalizika kabla ya magharibi
0 comments :
Post a Comment