MMILIKI wa timu ya Chelsea, Roman Abramovich, anatarajia kuonesha michoro ya ramani ya kuongeza viti vya Uwanja wa Stamford Bridge ambapo unatarajiwa kuingiza watazamji 60,000.
Maonesho ya wakazi kwenye mitaa ya London, yatakuwa ya kwanza kwa mashabiki wa timu hiyo kushuhudia jinsi uwanja utakavyokuwa na kwamba anataka kuweka historia uwe uwanja wa kipekee.
Majukwaa manne jinsi yatakavyobuniwa yatakuwa na muonekano wa kipekee ukilinganisha na viwanja vingi ambapo msanifu majengo atahakikisha kunakuwa na muonekano wa daraja lililosimama kwenye nguzo.
Kwa mujibu wa historia ya klabu hiyo kutoka kwa majirani zao, inaonesha wazo la ujengwaji wa Uwanja wa Kisasa wa Stamford Bridge kwa mara ya kwanza lilitolewa 1410 na imepita miaka 600 ndio unaanza kufanyiwa kazi.
Upanuzi huo kulingana na uchunguzi walioufanya lazima uwe na muonekano wa rangi ya bluu.
Mmiliki huyo ametenga paundi milioni 500 kwa ajili ya upanuaji wa uwanja huo.
0 comments :
Post a Comment