Mwongozaji wa video za muziki hapa nchini, Adam Juma, amewashauri wadau wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo fleva' wasiwe wepesi kuponda jitihada za wasanii wa hapa nchini, badala yake wakosoe kwa kurekebisha pale panapo stahili.
Akizungumza jijini Dar es salaam juzi, mwongozaji huyo, alisema ushauri huo unatokana na mapokeo kuhusu video mpya ya mkali wa muziki wa bongo fleva, Alikiba ya 'Chekecha Cheketua'
Juma, alisema baada ya video hiyo kutoka wiki hii, kumekuwa na maoni tofauti kutoka kwa mashabiki, huku wachache ndiyo wenye kuelewa kitu na wengine wanakurupuka kwa kuponda.
"Tunawavunja moyo sana wasanii, hata kama video ina mapungufu sio kusema mbovu, tatizo wadau hawajui kibaya na kizuri," alisema
Alisema katika sanaa kuna vitu vingi ambavyo wasanii wanapitia mpaka kufikia sehemu fulani na kwamba, wadau wasiwalazimishe wasanii hao kuruka hatua ambayo ndiyo msingi wa kazi zao.
"Mawazo yalio ambatanishwa na chuki hayajengi, yapo mapungufu lakini jitihada za Alikiba zinaonekana, tujifunze kutoa shukrani, kukosoa kwa kurekebisha na kutoa mwongozo sahihi," alisema
Hivi karibuni video ya wimbo wa chekecha cheketuaaliyotengeneza nchini Afrika Kusini ilirushwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku mashabiki wakitoa maoni yao mbalimbali..
0 comments :
Post a Comment