Rapa aliyewahi kutikisa dunia kwenye miondoko ya kufokafoka DMX amekamatwa na polisi kwa kosa la kumtelekeza mtoto bila kumpatia huduma zozote.
DMX alikamatwa nje ya ukumbi wa Radio City akijianda kuongoza hafla moja iliyokuwa ikifanyika ukumbini hapo sambamba na shaba ranks.
Inaelezwa kuwa mwanamke mmoja alimshtaki rapa huyo akimtuhumu kumwachia mtoto bila msaada wowote wakati akifahamu fika kuwa yeye hana uwezo.
Hii si mara yakwanza kwa rapa huyo kuingia kwenye mikono ya dola kwani mara kadhaa amekuwa akikamatwa kwa makosa ya wizi, matumizi ya silaha, dawa za kulevya, ulevi, ugomvi na mengineyo.
0 comments :
Post a Comment