.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Familia ya Messi, Aguero zavamiwa Chile


Familia ya mshambuliaji wa timu ya Argentina, Lionel Messi, juzi ilishambuliwa na mashabiki wa Chile huku mchezo wa fainali ukiendelea.

Familia hiyo ambayo iliwasili nchini hapo kwa ajili ya kumtazama nyota huyo katika mchezo wa fainali ya Copa Amerika dhidi ya wenyeji, ilijikuta na wakati mgumu baada ya kushambuliwa na baadhi ya mashabiki wa Chile. 

Wazazi wa Messi, Celia na Jorge, waliambatana na kaka wa mchezaji huyo Rodrigo na Matias, huku wakiamini kuwa watarudi nchini Argentina wakiwa na kombe, lakini Rodrigo alishangaa kuona anapigwa na shabiki baada ya kutoridhishwa na kitendo alichofanyiwa Messi dhidi ya beki wa Chile, Gary Medel kumpiga teke la tumbo.


Messi alionekana kuugulia maumivu ya tumbo ndipo kaka wa mchezaji huyo, Rodrigo alionekana akirushiana maneno na baadhi ya mashabiki na kisha kupigwa. Familia hiyo ilikuwa chini ya uangalizi wa polisi baada ya vurugu hizo ambazo zilitokea katika dakika ya 45 za mwanzo.

Familia hiyo ilichukuliwa na polisi kisha kuifadhiwa sehemu yenye usalama huku wakiangalia mchezo huo kupitia runinga.



Hata hivyo familia ya mshambuliaji wa timu hiyo, Sergio Aguero, nayo ilivamiwa na amshabiki wa Chile lakini polisi waliwahi kuwaokoa.

Mchezo huo ulimalizika huku Chile wakitwaa taji hilo kwa ushindi wa mabao 4-1 yaliopatikana kwa mikwaju ya penalti baada ya kumalizika dakika 120 bila ya kufungana.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad