Nigeria imetangaza kuachana na kocha wake, Stephen Keshi, baada ya kuripotiwa kuomba kazi ya kuifundisha Ivory Coast.
Nigeria ilitangaza juzi kuachana na kocha huyo aliyewapeleka hatua ya pili ya Fainali za kombe la Dunia mwaka jana.
Keshi 30, amekuwa na mgogoro mkumbwa na uongozi wa Super Eagles baada ya kuripotiwa kuwa alipeleka barua ya kuomba kazi ya kuifundisha Ivory Coast, ingawa amekuwa akikanusha kuwa hahusiki na barua hiyo.
Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), lilitangaza juzi kuachana na kocha huyo kutokana na suala la kuomba kazi hiyo nchini Ivory Coast.
"Kutokana na kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka la Nigeria kumkuta na hatia Keshi ya kuomba kazi ya kuifundisha Ivory Coast wakati bado ana mkataba na Eagles, tumeamua kuachana naye," ilisema taarifa kutoka kwenye mtandao wa NFF.
"Kutokana na hilo sasa timu ya taifa itakuwa chini ya Salisu Yusuf na mkurugenzi wa Ufundi atakuwa Shaibu Amodu, hadi hapo shirikisho litakapo tangaza vinginevyo."
0 comments :
Post a Comment