.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Ligi Daraja la Kwanza kuanza Sept. 12




Asha Kigundula
LIGI Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 inatarajiwa kutimua vumbi Septemba 12, mwaka huu, huku ikichezwa kwa makundi matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, alisema ligi hiyo itakuwa ya makundi matatu kutokana na marekebisho ya kanuni  yaliyofanywa hivi karibuni na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake kilichofanyika  Zanzibar.



Kizuguto alisema timu ya kwanza katika kila kundi la ligi hiyo itapanda kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kwa msimu wa 2016/2017 wakati timu itakayoshika nafasi ya mwisho katika kila kundi itashuka kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa msimu wa 2016/2017.

Kizuguto alisema katika Kundi A linaundwa na timu za African Lyon FC (Dar es Salaam), Ashanti United SC (Dar es Salaam), Friends Rangers FC (Dar es Salaam), Kiluvya United FC (Pwani), Kinondoni Municipal Council FC (Dar es Salaam), Mji Mkuu FC (Dodoma), Polisi Dar es Salaam na Polisi Dodoma.

Kaundi  B ni Burkina Faso FC (Morogoro), Kimondo SC (Mbeya), Kurugenzi Mafinga FC (Iringa), Lipuli FC (Iringa), Njombe Mji FC (Njombe), Polisi Morogoro na Ruvu Shooting (Pwani).

Wakati Kundi C ni Geita Gold SC (Geita), JKT Kanembwa FC (Kigoma), JKT Oljoro (Arusha), Mbao FC (Mwanza), Panone FC (Kilimanjaro), Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers (Tabora).
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad