.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Mtitu awatilia shaka wasanii watangaza nia


Msanii na msambazaji wa filamu nchini, William Mtitu, amesema hana uhakika na wasanii wote waliojitokeza kutangaza nia ya kuwania nafasi mbali mbali za ubunge na udiwani kaika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu (2015), akieleza wapo wenye nia ya dhati na wengine wanaangalia maslahi yao.



Akizungumza na Mtanzania juzi, Mtitu ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji wa filamu za Kibongo '5 Effects Movies Ltd', alisema anaamini baadhi walio na nia thabiti ya kuwatumikia wananchi huku wengine wakitumia mwanya huo kujitafutia umaarufu.



Kwenye msafara wa mamba hata kenge wamo, ndivyo ilivyo kwa sasa kwa wasanii wanaojitokeza kuwania nafasi mbali mbali za uongozi, wapo wanaotafuta maslahi na si kuwatumikia wananchi kama wanavyojinadi," alisema



Aidha Mtitu aliwataka wote waliotangaza nia wanaotoka kwenye tasnia ya filamu endapo watapata nafasi ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wawe mfano wakuigwa na wasimamie haki za tasnia hiyo.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad