MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Linah Sanga amesema katika wimbo wake mpya ambao amefanya na Christian Bella ilibidi afute mistari yake ili kwenda sawa na msanii huyo baada ya kuona amefunikwa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Linah alisema Wimbo wake wa 'Hello' alifanya na mwanamuziki, Khadja Nitto lakini baadhi ya wadau walimshauri kuwa angefanya na mwanamuziki wa kiume hivyo wadau hao walimpendekeza Christian Bella afanye naye wimbo huo.
Alisema alikuwa anamuogopa Bella kwasababu ni mwanamuziki mkubwa na alikuwa anajiuliza anamuanzaje na anamuingiaje, ili kufanya naye hiyo kazi hivyo.
"Nakumbuka siku ambayo mimi nilikuwa nimesafiri Imma ze boy alinipigia simu na kunipa taarifa kuwa Bella alikuja studio kufanya ile kazi ambayo tulikuwa tumekubaliana kufanya hivyo nilikuwa na furaha kupata taarifa hizo," alisema.
"Niliporudi na kusikiliza ile kazi kweli nilikuwa nimefunikwa kabisa, na baadhi ya watu waliosikiliza kazi ile nao waliniambia kuwa nimefunikwa, hivyo nilichokifanya nikarudia upya kufanya ile kazi hivyo unaposikia 'Hellow' ya sasa si vitu nilivyokuwa nimeimba kwa mara ya kwanza," alisema.
0 comments :
Post a Comment