Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nuh Mziwanda amesema anamuamini Munguna yeye hana imani na mambo ya Kishirikina.
Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni baada ya baadhi ya mashabiki wakidai kuwa msanii huyo anajihusisha na imani za kishirikina kwa kutumia alama ya 666 katika mitandao yake ya kijamii jambo ambalo limemfanya kungara kwenye tasnia hiyo.
Nuh anasema anamuamini Mungu hana imani hizo na haamini kama namba hizo (666) zinatumika na watu wanao amini ushetani kwani kila kitu ni imani kama zilivyo imani zingine.
Anasema haamini katika hizo namba amabazo baadhi ya mashabiki wake wamesema na kwamba kitu kikiaminiwa kinaweza kumdhuru mtu lakini kwa upande wake haamini hilo.
Katika hatua nyingine Mziwanda anasema anatarajia kufunga ndoa na shilole kwa sababu anaamini wanapendana ndiyo.
0 comments :
Post a Comment