Milipuko miwili katika mkutano wa hadhara wa amani katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara umeua watu wasiopungua 86 kujeruhi 186, kwa mujibu wa viongozi.
Tv zilionesha watu wakiwa na hofu huku wamelala chini wakitokwa na damu wakiwa na mabango ya maandamano.
Milipuko hiyo imetokea karibu na kituo kikubwa cha treni ambapo watu walikuwa wamekusanyika kufanya maandamano.
Tukio hili ndo shambulizi kubwa kuwahi kutokea katika ardhi ya Uturuki na idadi kubwa ya vifo.
Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu ametangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa na kuna ushahidi kwamba mabomu hayo yalibebwa na wajitoa muanga wawili.
Mabango yaliokuwa yakitumika kwenye maandamano yalitumika pia kufunika mili.
Raisi Recep Tayyip Erdogan alisema shambulio hilo, amablo limekuja wiki kadha kabla ya uchaguzi lilikuwa tendo la kigaidi na kutengeneza chuki.
Mkutano huo wa hadhara wa kudai kumalizika kwa ghasia kati ya Wanamgambo wa PKK na serikali ya Uturuki, na ilipangwa kuanza saa 12:00 kwa saa za Uturuki.
Huko Istanbul wandamaji wakiwa wanapinga shambulio hilo katika mitaa mbalimbali
SHUKA CHINI KUANGALIA VIDEO YA JINSI BOMU LILIVYOLIPUKA
Source: BBC
0 comments :
Post a Comment