.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Ommy Dimpoz awapa Somo Wasanii Wenzake



Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu hapa nchini wamekuwa na tabia ya kuweka mambo yao ya Mahusiano hadharani kwa kuandika kwenye mitandao ya kijamii na hata wakati mwingine kutupia picha.

Hata hivyo hatua hiyo inaonekana kumkera msanii wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' na amewataka kujifunza kutunza siri za mahusiano yao.


Msanii huyo alisema kuwa hafurahii kuona tabia hiyo ya kuweka wazi mpenzi wake na kwamba huo ni mtindo wa wasanii wa nje ambao unaendana na maadili tamaduni zao.



"Wanaomfahamu mpenzi wangu ni watu wa karibu na mimi sio kila mtu kwani mambo ya mapenzi kwa kawaida huwa ya siri na sio kuweka hadharani kama ambavyo wasanii wenzake wamekuwa wakifanya.

Maisha yangu yataendelea kuwa binafsi na muziki wangu utakuwa kwa mashabiki wangu wote kwa kuwa unawahusu wao na sio mahusiano ya kimapenzi ambavyo naamini ni yangu binafsi." alisema Ommy
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad