Wakati imeripotiwa kuwa klabu ya Yanga imepanga kumuuza kiungo Andrey Coutinho, uongozi wa klabu hiyo umesema Mbrazil huyo anakwenda kucheza soka la kulipwa barani Asia katika timu ambayo itatangazwa baada ya mipango ya usajili kukamilika.
Vyombo vya habari viliripoti wiki iliyopita kuwa kiungo huyo alikuwa anatakiwa na klabu ya St George ya Ethiopia, lakini katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha amefunga na kueleza hakuna mpango huo.
Tiboroha alisema juzi kuwa kiungo huyo tayari ameshatimkia barani Asia kwa ajili ya kukamilisha taratibu za usajili.
"Coutinho hayupo nchini, kama timu zinamuhitaji, wanaweza kumfuata aliko na kumsajili," alisema Tiboroha.
"Timu iko kambini Bagamoyo inaendelea kujifua chini ya Kocha Mkuu Hans van Pluijm na Juma Mwambusi kuendelea na maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Mgambo Shooting Jumamosi," alisema Tiboroho
0 comments :
Post a Comment