.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

HABARI KAMILI NA ZA KINA KUHUSU KUGOMBANA KWA P-SQUARE


Wiki hii mitandao ya nchini Nigeria iliripoti kuwa kulikuwa na ugomvi Mkubwa kati ya mapacha wawili wanaounda kundi la P Square,Peter na Paul Okoye na kwamba walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezi.
Habari zilichochewa na tweet hii ya kaka yao Mkubwa ambaye pia ni Meneja wao,Jude Okoye

tweet hii  iliyotafsiriwa na mitandao hiyo huenda ameachana na kundi hilo.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo aitwaye Bayo Adeta alikanusha Habari hizo wakati akihojiwa na Premium Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo zimetoka wapi.
Kupitia juhudi za BLOG YA VIJANA tuliweza kupata kuona taarifa kutoka kwa mtu wao mwingine wa karibu alisema maneno haya kwa kingereza na pia tafsiri kwa lugha ya kiswahili utaweza kusoma baada ya maneno haya ya kingereza...


Maneno hayo yaliosemwa na mtu wa karibu unaweza kuyasoma kwa kiswahili hapa chini...Tafsiri na (Blog ya Vijana- email- blogyavijana@gmail.com)

"Ndio wamepigana wiki hii, Peter ameacha alama kwenye jicho la kushoto la Paul, ila ugomvi huo haukua muda wa mazoezi, Mazoezi gani? Peter amegoma kufanya kitu chochote kuhusiana na P-Square kwa wiki. Sahau kuhusu kuwepo kwenye harusi ya kaka yake, ila mambo hayapo vizuri baina yao kwa sasa. Peter anataka kutoka. Amesema Paul na Jude wanamtenga yeye, Kwamba wakitoa nyimbo 200 basi 199 zitakua nyimbo ambazo amefanya Paul, mpaka watu wanamuona kama yeye mchezaji ndani ya P-square. Peter amechukia sana, ni mtu safi sana na rafiki wa watu, Pia amemtuhumu kaka yake Jude kwa kosa la kutomheshimu mke wake Lola kwa miaka mingi na amechoka kuendelea kuona hivyo. Hata hivyo Peter amesema kwamba sio tu Lola ni mkubwa kwa Jude ila pia ni Mjamzito na Jude amekuwa akimkasirisha mwanamke mjamzito. Kama ulikua makini Jude akuhudhuria harusi yao mwaka jana hata kama alikua Nigeria. Jude alimuuliza Peter kwanini hakumuoa Lola wakati mama yao yupo hai. Jude amesema ni mke wake anae msukuma peter na wanatakiwa kumuombea. Inasemekana hakuna mtu katika familia ya OKoye anampenda Lola na hawakushinikiza ndoa yao. Makaka hao wamekasirikiana sana, hata mapolisi wanahusika sasa, wiki mkubwa wa mapolisi au mtu kutoka ofisini alitembelea nyumbani kwao.

Kitu kibaya ni kwamba wamemwita wanasheria aje kugawanisha mali zao, wanataka wagawane kila kitu. Mwanasheria alikua kwao nadhani Alhamisi. Peter alisema hakuna tena kushirikiana kwa P-Square, Unajua wanamiliki kila kitu pamoja pamoja na nyumba iliopo Omole, Parkview na Atlanta. Mambo yasipofanyika haraka basi P-square inakaribia kufa. Najua watu wamekuwa wakiingilia na kuomba sana waelewane, kwamba wao ni kundi kubwa sana hapa Afrika, hakuna atae faidika kama wakitengana. Nguvu ya wao kutengeneza pesa ipo kwenye umoja wao. 
"Ni jude amabe watu wanamuomba awapatanishe makaka hao, lakini baada ya alichokiandika twitter hapo jana inawezekana ndo ikawa mwisho wa P-Square. Jude amejitahidi sana kwa ajili ya kaka zake mpaka kufikia hatua ya kuacha vitu vingi kwa ajili yao.


Jude amesimamisha maisha yake binafsi kwa ajili ya kaka zake. Aliuza gari lake lakwanza ili waweze kushoot video yao yakwanza ila yote hayo yamefikia mwisho wake kama alivyo andika twitter. Kitu kinachoweza kuweka mambo sawa ni labda maajabu yatoke Jude na Lola waondoe tofauti zao, ila sioni hilo likitokea



Source; BLOG YA VIJANA Endelea kupata habari za kina zaidi hapa ili kuwa mwana familia wa Blog hii na kuweza kupata habari punde tu zinapotokea like page yetu ya facebook kwa kubonyeza hapa BLOG YA VIJANA ni bure kabisa
Share on Google Plus

About Blog Ya Vijana

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

ad