Kuna barua nyingine tena zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa wa Kitanzania wanaotumikia vifungo vyao huko Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya. Anayechapisha barua hizo kwenye mitandao anadai eti ni za kweli na zinatoka kwa wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani huko Hong Kong. Anadai kuwa yeye ni padri na huwa anaendesha ibada magerezani. Anadai huwa anatembelea magereza ya Hong Kong karibu kila siku ambapo hukutana na wafungwa wa Kitanzania.
Naomba nimnukuu kama alivyoandika yewe mwenyewe baada ya mchangiaji mmoja kwenye tovuti husika kumhoji kuhusiana na ukweli wa hizo barua.
Kuhusiana na wafungwa wa madawa ya kulevya huko Hong Kong Balozi Marmo alishawahi kusema kuwa idadi ya Watanzania walio katika magereza na mahabusu huko China, Hong Kong na Macao, inatisha. Alipoulizwa hatima ya Watanzania hao, Balozi huyo amesema, “Tunawapa ushauri nasaha kwa sababu kuna udanganyifu mkubwa kwenye magereza hayo (walimofungwa), wengine wanaambiwa kwamba kuna uwezekano wa kuwarejesha nyumbani ili wamalizie vifungo vyao, lakini huwa tunawaambia hili jambo haliwezekani kwa sababu Tanzania na China, Tanzania na Hong Kong na Tanzania na Macao hatuna mikataba ya kubadilishana wafungwa.
“Na wala hatuna sasa hivi uwezekano wa kufanya jambo hili kwa sababu mzigo ni mkubwa, laiti ingepita miaka miwili au mitatu bila kuwa na mtu au mhalifu wa kuleta dawa za kulevya, tungekuwa na mjadala na mataifa haya.” Anasema Balozi Marmo, “Kunakuwa na uchunguzi mkali sana, unachukua wakati mwingine hadi miaka mitatu. Hujui (hao watuhumiwa) wanazielezea nini mamlaka za hapa.”Zipo barua tatu. Barua ya kwanza inadaiwa kuandikwa na mfungwa Agosti 9, 2013 kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete. Barua ya pili haina tarehe. Barua ya tatu inadaiwa kuandikwa Agost 8, 2013 kwenda kwa Dr. Mwakyembe na imeoothoresha majina ya wanaodaiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulenywa, yakiwemo majina ya viongozi wa kidini. Again, sina uhakika kama waliotajwa wanahusika na hiyo biashara. Mie nimekopi na kupaste tuu habari kama nilivyoikuta. kama yaliyoandikwa kwenye hizo barua ni ya kweli au uongo kwa kweli ni vigumu sana kujua.
0 comments :
Post a Comment