Mashabiki mbalimbali wamemuuliza Dillish kuhusu Guyo kupitia twitter, lakini Dillish ambaye ameonesha kushangazwa na habari hizo, saa moja iliyopita ametweet kuwa baba yake ana asili ya Somalia hivyo hajui huyu jamaa ameibukia wapi!
Bwana Guyo ambaye ni askari mstaafu wa Kenya alisema alikuwa ni miongoni mwa maaskari wa Kenya wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa ‘United Nations Transition Assistance Group ‘, kilichopelekwa nchini Namibia kuanzia (April 1989) mpaka (March 1990) kusimamia mchakato wa amani pamoja na uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo na huko ndiko alikutana na mama yake Dillish aitwaye Selma na wakapendana.
Kwa mujibu wa Standard Media, wiki iliyopita mwandishi wa Namibia Rinelda Mouton alifanya mahojiano maalum na Dillish Mathews, ambaye alisema anatamani kukutana na baba yake mzazi.
0 comments :
Post a Comment