Taarifa ya shirikisho hilo imesema katika mchezo
huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3,
mashabiki 57,422 ndio waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo la kukata
na shoka ambalo viingilio vyake vilikuwa Sh5,000, Sh7,000, Sh10,000,
Sh15,000, Sh20,000 na Sh30,000. “Ni tiketi 131 tu ndizo ambazo
hazikuuzwa.

Kati ya hizo 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo uwanjani hapo,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kila klabu imepata mgawo wa Sh123.1 milioni wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni Sh76.4 milioni.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya Uwanja (Sh62.6 milioni), gharama za tiketi (Sh7.3 milioni), gharama za mechi (Sh37.6 milioni), Kamati ya Ligi (Sh37.6 milioni), Mfuko wa Maendeleo ya Soka (Sh18.8 milioni) na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (Sh14.6 milioni).

0 comments :
Post a Comment