Muigizaji na mwimbaji nchini Kitale yuko Tanga alipoenda
kuhudhuria Dua ya kumuombea marehemu Sharo Milionea ikiwa ni mwaka mmoja
tangu afariki dunia kwa ajali mbaya ya gari.
Kitale ambaye ndiye msanii pekee aliyefika Tanga siku ya juzi amesema
kuwa amejifunza mambo mengi katika msiba wa rafiki yake Sharo Milionea,
ikiwa ni pamoja na misiba ya wasanii wengine waliotangulia mbele ya
haki, Kanumba na Sajuki.
Akiongea kwa njia ya simu na Edson Mkisi katika kipindi cha Hatua
Tatu cha 100.5 Times Fm, Kitale amesema kutokana na funzo alilopata
ameampa ujumbe mama yake ili kwamba pindi atakapotangulia mbele ya haki
mambo hayo yasijirudie kwake.
“Nimejifunza vitu vingi na nimejua marafiki walio wema na marafiki
wasio wema. Ina maana kwamba kuna marafiki wanafiki na marafiki wasio
wanafiki. Amesema Kitale.
“Kuna vitu vingi nimejifunza baada ya kuondoka marehemu Steven
Kanumba, nimejifunza baada ya kifo cha Sharo Milionea, na nimejifunza
baada ya kifo cha Sajuki. Nimejifunza vitu vingi sana sana sana.”
Amesisitiza.
“Ina maana hata mimi kama ntatangulia kuna mambo ambayo
nimeshamweleza mama yangu na nimeshaieleza familia yangu, nafikiri
hakitakuja kutokea kama kilichotokea kwa wenzangu. Nimejifunza vitu
vingi hasa ukiwa msanii...” Kitale ameiambia Hatua Tatu.
Hata hivyo Kitale alikataa kueleza ujumbe huo na kudai kuwa ni siri
kati yake na familia yake kwa kuwa hafahamu nani atatangulia kati yake
na wazazi wake.
Kitale amewashauri wasanii kumkumbuka Mungu wakati wanapoendelea na
shughuli zao na ndio sababu watu wengi wanaamini kuwa asilimia kubwa ya
wasanii ni ‘Freemason’, na kwamba hiyo inatokana na kitendo cha wasanii
hao kumsahamu Mungu wao.
Siku kama ya jana mwaka uliopita (November 27,2012) ndio siku ambayo marehemu Sharo Milionea alizikwa huko Tanga.
0 comments :
Post a Comment