.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Jose Mourinho 'akubali' kuvaa viatu vya Van Gaal



Kocha Jose Mourinho, yupo tayari kuvaa viatu vitakavyoachwa na Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal endapo kama atatimuliwa.

Van Gaal yupo kwenye wakati mgumu Old Trafford baada ya kufungwa mabao 2-1 na Norwich City kwenye Ligi Kuu England na kuifanya timu hiyo kucheza mechi tatu kati ya 13 katika mashindano yote bila kupata ushindi.

Pamoja na kupigwa kura za siri ndani ya uongozi wa United kwa saa 48 zijazo, kipigo hicho cha mwishoni mwa wiki kimebadili mawazo ya bodi ya timu hiyo Old Trafford.

Kutokana na Mourinho kutimuliwa na Chelsea wiki iliyopita, Mreno huyo yupo katika nafasi ya juu kwenye orodha ya makocha watakaorithi mikoba ya van Gaal akiwa pamoja na msaidizi wa sasa wa timu hiyo, Ryan Giggs.

Na inaelezwa kwamba Mourinho, ana nafasi ya kutua Old Trafford na yupo tayari kuina timu hiyo huku akiwaeleza marafiki zake kwamba kuna kazi nyingine ni ngumu kuzitosa.

Van Gaal atakuwa kwenye wakati mgumu zaidi endapo United haitopata matokeo mazuri dhidi ya Stoke City jumamosi na mechi inayofuata dhidi ya Chelsea.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad