.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

UCHAMBUZI WA MECHI YA ARSENAL VS LIVERPOOL




Mchezo huu ulianza kama mkutano wa Timu za Pande mbili zinazoongoza Ligi la England na Arsenal walionesha uwepo wao na umakini wao wa kuendelea kushikilia namba moja kwenye ligi kwa kua walikua na Advantage kutokana na kufungwa kwa Chelsea 


Saint Cazorla alifanya Arsenal kuwa mbele kwa Goli mmoja baada ya kuonesha kuwa yeye ni winga mzuri kwa kupiga kichwa kizuri sana bahati mbaya mpira ukagonga mwamba na kisha yeye mwenye kumaliza kwa shuti kali sana... Kisha Aaron Ramsey akafunga Goli la 10 kwenye Campaign yake kwa shuti moja kali nje ya boksi kubwa...


Luis suarez aligongesha mwamba baadae lakini huu ulikua ushindi wa kuridhisha kwa upande wa Arsene Wenger wakiwa ndo wanafuta majonzi ya kupigwa na Chelsea katikati ya wiki kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani
 
Matokeo haya sio ya kuridhisha kwa Kocha wa Liverpool Brendan Rodegers baada ya kusafiri mpaka Kaskazini mwa London na matumaini ya ushindi akiwa amenza msimu huu vizuri sana 

Cazorla na Ramsey waomba sana posho yao ya magoli hayo yalioifanya Arsenal kuchukua point zote tatu, lakini Kaptain wao Mikel Arteta ameonesha kiwango cha juu yeye kama kiungo wa kati na kaptain wa timu aliweza kuwamudu liverpool pale kati na pia kutengeneza njia rahisi ya kwenda kupata magoli hayo.....

Liverpool walipata tabu sana upande ya nyuma (mabeki) baada ya beki wa Timu ya Taifa ya England Glen Johnson kutolewa baada ya kuumia. Ilimpatia nafasi kijana mdogo Jon Flanagan ambae hajawahi kucheza ligi la England tangu lianze, mara yake yamwisho kucheza ilikua mwezi wa nne 2012


 Arsenal walicheza bila Jack Wilshere amabe ni majeruhi lakini kulikua na mpira mzuri sana kutoka [pande zote mbili na kufanya kipindi cha kwanza kunoga na mashabiki kukifurahia sana


Kipa wa Liverpool Simon Mignolet alianza mapema kuokoa mipira iliokua inapigwa na Tomas Rosicky, huku Jordan Henderson alionekana mwenye mshangao kwa jinsi alivyokua akipita mabeki wa Arsenal bila ya patashika yeyote na kupiga mashuti kwa kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny


Arsenal walitumia dakika 19 tu na kupata goli lao lakwanza kupitia kwa Cazorla ambae alitua njia zake mbadala na aliweza kumudu nafasi yake vizuri baada ya kupiga mpira kichwa na kugonga mwamba ndipo alipoweza kumtoka Mignolet na kumalizia mpira huo kwa shuti kali sana


Liverpool walijiona sio wenye bahati baada ya refa Martin Atkinson kuwakatalia goli lao ambalo Jordan Herderson alimalizia baada ya kupewa pasi na Daniel Sturridge, Suarez aliangushwa na Bacary Sagna na filimbi kuashilia ni faulo lakini kwa haraka sana Suarez alituliza mpira chini na kumpigia Sturridge ..Lakini kwa haraka io Refa alikata goli hilo na kusema Faulo ipigwe vizuri


Arsenal walitengeneza nafasi za hatari nyingi sana lakini Giroud alishindwa kuzitumia ipasavyo baada ya Mchezaji wa zamani wa Arsenal ambae kwa sasa yupo Liverpool Kolo Toure kupoteza pasi lakini Giroud alipiga mpira huo moja kwa moja kwa kipa

Arsenal walikua awafanyi makosa maeneo ya golini kwao .... ilipofika dakika ya 59 Ramsey aliwafanya Liverpool walipe mda walio upoteza kwa kupiga shuti kali sana kutumia mguu wa kulia  umbali ya hatua 25 kutoka golini iliompita kwa juu Mignolet


Kocha wa Liverpool amesema Arsenal walikua bora zaidi yao

 UCHAMBUZI BY : FEISAL J.PINTO 0712 225486
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad