KIUNGO wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’, amesema kuwa iwe isiwe,
lazima astaafu na taji kubwa au ubingwa kwenye timu ya Taifa na hata
klabu yake.
Chuji alisema atahakikisha anapata mataji makubwa akiwa na timu hizo ili akistaafu, afanye hivyo akiwa na rekodi mkononi.
“Umri unaenda na itafika wakati nitasema sasa soka
basi, lakini cha msingi inafaa mtu kuangalia ni mafanikio gani umepata
kwenye kazi yako ya soka na kipi utajivunia zaidi kama mchezaji, hivyo
ninataka kuisaidia timu yangu kupata taji kubwa ili siku nikistaafu niwe
na rekodi,” alisema.
“Naamini nikiwa na timu ya taifa na hata kwenye kikosi cha Yanga, lazima nijitahidi ili kufanikiwa.”
Kuhusiana na muda wa kustaafu, alisema bado
hajafikiria ni wakati gani atastaafu, akisisitiza: “Kwa sasa bado niko
fiti na mwenye afya njema.”
Chuji yuko Kenya na kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, kinachoshiriki mechi za Kombe la Chalenji.
0 comments :
Post a Comment