Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake Gangilonga Iringa leo kwa heshima za mwisho |
Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com juu ya kifo hicho katibu msaidizi mkoa wa Iringa Jimson Mhagama alisema kuwa Mteming'ombe alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa figo na athima
Alisema kuwa Mteming'ombe alikuwa amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa zaidi ya siku tatu sasa akitibiwa .
Hata hivyo alisema kuwa maradhi hayo yalimfanya kushindwa kufika ofisini toka Novemba 27 mwaka huu siku ambayo mkoa wa Iringa ulipata kuhitimisha mbio za bendera .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema kuwa kifo cha katibu huyo kimeacha pigo kubwa kwa chama hasa ukizingatia kuwa mchango wake ulikuwa ukihitajika sana katika uhai wa CCM mkoa wa Iringa.
Msambatavangu alisema kuwa mazishi ya katibu huyo yanataraji kufanyika kesho Desemba 20 katika kijiji kwake Mageha mjini Rujewa wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya .
Alisema kuwa miongoni mwa viongozi wa CCM Taifa wanaotarajia kushiriki mazishi hayo ni pamoja na naibu katibu mkuu wa CCM Mwingulu Nchemba na viongozi mbali mbali wa chama na serikali kutoka ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa.
Msambatavangu alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa itaendelea kumuenzi Mteming'ombe kwa kuendeleza yale yote aliyeyatenda katika chama mkoa .
Huku mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akizungumzia juu ya kifo hicho alisema kuwa alipokea kwa mshituko mkubwa taarifa ya kifo hicho baada ya kupokea simu majira ya saa 8 usiku .
Kiponza alisema kuwa CCM mkoa na taifa imempoteza kiongozi mchapakazi ambaye katika uongozi wake alikuwa na ushirikiano mzuri kwa kila mmoja bila kubagua .
Miongoni mwa viongozi wa chama na serikali mkoa wa Iringa waliofika nyumbani kwa marehemu Gangilonga Iringa kutoa heshima zao za mwisho jana ni pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma, katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayub , meneja wa Tanroad mkoa wa Iringa Paul Lyakurwa ,mjumbe wa NEC mkoa wa Iringa Mahamud Madenge , kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa salim Asas, kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri na wengine wengi
Mdogo wa marehemu Bw James Mteming'ombe alisema kuwa marehemu alizaliwa mwaka 1956 na kuwa ameacha mke mmoja na watoto watatu.
0 comments :
Post a Comment