Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania
Hoyce Temu akipozi mara baada ya kulamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili
wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini
Mwanza.
Hoyce Temu akipata Ukodak na Mdau wa tasnia ya habari nchini.
Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.
Pongezi pia ziende kwa Dada Lulu Musa Afisa
Uhusiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kulamba Nondozz ya
shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika chuo cha St. Augustine
University kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini
Mwanza mwishoni mwa Juma.
Mbali na kula Nondozz kwenye siku hiyo
maalum Hoyce Temu ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na
Tanzania aliamua kufanya mahojiano na baadhi ya wahitimu kwa ajili ya
kipindi chake.
Mlimbwende Hoyce Temu akizungumza na
mwandishi wa habari wa ITV kuhusiana na taalum aliyoipata itakavyoweza
kuboresha utendaji wake kazini pamoja na kuendelea kuisaidia jamii
inayomzunguka kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania.
Mwanandishi wa habari wa kituo cha ITV Shaban Tole akimpongeza Hoyce Temu.
Hoyce Temu katika picha ya kumbukumbu na marafiki.
Hoyce Temu akiondoka eneo la tukio na furaha isiyo na kifani.
0 comments :
Post a Comment