kiungo wa Man United Shinji Kagawa
KOCHA Mkuu wa Manchester United, David Moyes
amefichua kwamba kiungo Shinji Kagawa alikula kupita kiasi na hivyo
kuugua hadi kukosa mechi ya juzi Jumamosi dhidi ya Newcastle United
kwenye Ligi Kuu England.
Kiungo huyo wa Japan alikula na kufanya tumbo lake
kujaa kupita kiasi na kushindwa kupumua baada ya mechi ya kipigo dhidi
ya Everton Jumatano iliyopita.
Kagawa aliwahishwa hospitali usiku huo huo baada ya kulalamika kwamba anashindwa kupumua vizuri.
Akizungumza baada ya mchezo wa kipigo cha bao 1-0
kutoka kwa Newcastle United juzi Jumamosi, Moyes alisema, “Shinji
alikuwa anaumwa sana baada ya mechi ya Everton na alifanya mazoezi
makali Ijumaa, lakini kwa sasa amepata nafuu.
“Ulikuwa ni ugonjwa mbaya. Nadhani alikula kupita kiasi na tumbo lake likajaa, lakini kwa sasa yuko vizuri.”
Kwenye mechi hiyo, Kagawa alitolewa katika dakika
58, lakini alianza kujisikia vibaya wakati akirudi nyumbani kwake
Alderley Edge, Cheshire.
0 comments :
Post a Comment