KIPA mpya wa Yanga, Juma Kaseja jana alianza rasmi mazoezi na kikosi chake kipya kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara na michuano Klabu Bingwa Afrika.
Kipa huyo alitua kwenye mazoezi ya Yanga kwa
staili ya kuchimba mkwara akionyesha kwamba yuko tayari kuchapa mzigo na
kukabiliana na changamoto zozote.
Kaseja aliyeichezea Simba kwa takriban miaka 10,
amejiunga na Yanga kwa mara nyingine na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Aliwahi kuichezea Yanga mara ya kwanza mwaka 2008.
Alianza rasmi mazoezi na timu hiyo jana Jumatatu
kwenye Uwanja wa Boar, Dar es Salaam na alisisitiza kuwa amepona kabisa
tatizo la kifundo cha mguu lililokuwa likimsumbua tangu wiki iliyopita
na sasa yuko fiti.
Katika mazoezi hayo Kaseja alionekana mchangamfu isivyo kawaida na hakuonyesha ugeni wowote.
Muda mwingi alikuwa akipiga stori na kufurahi na wenzake huku akionyesha hali ya kujiamini.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja alisema
amefurahi kuanza mazoezi Yanga na amevutiwa na mazoezi hayo licha ya
kuwa ni siku yake ya kwanza.
“Lakini jambo la kwanza kubwa ninalowaambia
wapenzi wa Yanga, mimi ni mtu wa vitendo na si mzungumzaji nje ya
uwanja, pili, ili mambo yaende vizuri nahitaji sana sapoti ya mashabiki,
viongozi na wachezaji wenzangu lakini tatu wafahamu kuwa mimi kama kipa
wao siko tayari kuwaangusha ila wakubali kuwa mpira una mambo matatu
ambayo ni kushinda, sare na kufungwa,”alisema baada ya kuulizwa ni namna
gani ataweza kukabiliana na changamoto za mashabiki ambao wamekuwa na
tabia ya kulaumu makipa wanapofungwa.
Aliongez: 'Waone kuwa mpira ni kazi ya watu kama
zilivyo kazi nyingine,nilikuwa Simba na sasa niko Yanga lakini eti kwa
sababu zamani nilikuwa kule nitashindwa kufanya kazi yangu si
kweli,wajue kuwa,upenzi upo hata Ulaya lakini makipa wao wanapofungwa
inakuwa sehemu ya mchezo na siyo kuwalaumu na hakuna anayependa kufungwa
aharibu kazi yake,”alisema Kaseja.
Akizungumzia mazingira aliyoyakuta jana baada ya
kuanza kazi hasa kunolewa na kocha mpya kwake, Razack Siwa kipa huyo
alisema: “Nimefanya na kocha, Siwa nafikiri ni mzuri ingawa kwa sasa ni
mapema mno kuzungumzia tofauti na yule aliyekuwa ananifundisha Simba,
James Kisaka.”
Siwa alisema: “Kaseja ni kipa mzuri na nafikiri ataisaidia timu, tumeanza naye leo (jana) anafanya vizuri.”
Kocha mku wa Yanga, Ernest Brandts alisena:
“Kaseja ni kipa mzuri kama unavyojua Yanga, inapenda kuwa na wachezaji
wazuri na ndiyo maana yupo hapa.
0 comments :
Post a Comment