TUME
ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), imepata pigo baada ya Mamlaka ya
Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA), kuizuia isitoe zabuni za kuandaa vifaa
vya uchaguzi vya kielektroniki kwa kampuni za M/S Jazzmatrix Cooperation
na M/S Invu IT Solution zenye thamani ya sh bilioni 126.3.
PPAA imefikia hatua hiyo baada ya kampuni za M/S Morpho na M/S IRIS Corporation Technology kukata rufaa kupinga uamuzi wa NEC kutoa zabuni kwa kampuni hizo.
M/S Morpho ililalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo iliyoahidi kuifanya kwa sh bilioni 97.8 lakini zikapewa kampuni zilizoahidi kuifanya kwa sh bilioni 126.3.
Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa PPAA, uamuzi huo ulifikiwa mwezi uliopita ambapo NEC imeamriwa kurudia upya mchakato mzima wa kutoa zabuni, ikiwemo kutangaza katika vyombo mbalimbali vya habari kwa utaratibu unaokubalika.
Mkakati wa NEC kutoa zabuni kwa kampuni hizo uliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ambapo alisema ulikuwa na lengo la kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.
Zitto alisema lengo ni kuhakikisha mchakato wa vitambulisho vya kupigia kura vya kielektroniki vinakuwa na faida kwa CCM na kukiingizia fedha chama hicho za kutumia kwenye uchaguzi huo kupitia mfumo huo dhaifu wa vitambulisho hivyo.
Kampuni zilizokosa tenda zililalamika kwa mkurugenzi wa NEC namna mchakato wa kutoa zabuni hiyo ulivyoendeshwa, na kwamba ulikuwa haujawatendea haki ikiwa ni pamoja na kutofahamishwa sababu zilizowafanya wakose kazi hiyo.
Kampuni hizo zilihoji njia na sababu zilizowafanya wakose tenda hiyo licha ya kuwa na uzoefu, vifaa bora pamoja na kuwa na kiwango kidogo cha gharama tofauti na kampuni iliyopewa kazi.
Katika moja ya malalamiko yao, Kampuni ya M/S Morpho ililalamika kutofahamishwa namna walivyokosa vigezo vya kupata kazi hiyo licha ya kuwa na sifa za kimataifa za kufanya kazi, huku ikiwa imetoa bei nafuu kuliko kampuni iliyopata kazi.
“Tulikuwa miongoni mwa washindani muhimu kwa kuwa kiwango chetu kilikuwa ni sh bilioni 97.8 ambazo ni sawa na euro 44,939,912, ujuzi, vigezo na uzoefu wetu havilingani, duniani kote tumefanya kazi katika maeneo mengine kwa ufanisi na tunashindwa kuelewa kivipi walishinda hao ambao wamepata kazi kwa kiwango cha zaidi ya sh bilioni 27.8 ikilinganishwa na yetu,” ilisomeka sehemu ya barua yao ya malalamiko waliyopeleka NEC.
Tanzania Daima Jumatano, lilimtafuta Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, ambaye hata hivyo hakuwa tayari kueleza hatua watakazozichukua dhidi ya uamuzi huo.
“Siwezi kuliongelea suala hilo kwenye simu…nakuomba ndugu yangu tuonane kesho nitakupa ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo,” alisema.

0 comments :
Post a Comment