MREMBO anayedaiwa kuliingilia penzi la staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu
na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliyewahi kushiriki Shindano la
Miss Tanzania, Amisa Mabeto amefunguka kuwa
mwanamuziki huyo ni shemeji yake tu, hakuna chochote kati yao.
Akipiga stori na safu hii kuhusiana na madai hayo, Amisa alisema
alistaajabu kwani hana mazoea na Diamond Kama ni kuonana waliwahi
kuonana miaka ya nyuma, tena siyo kimapenzi.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Kamwe siwezi kutembea na Diamond na haitatokea kwani jamii nzima inajua
yupo na Wema na mimi huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa, hana chake hapa,
siwezi kutembea naye kamwe, namheshimu kama shemeji yangu,” alisema
Amisa.
Amisa aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano na Diamond akiwa ni shosti mkubwa wa Wema.
0 comments :
Post a Comment